ALI KIBA AINGIA ANGA ZA CHRIS BROWN
MSANII wa muziki wa bongofleva Ali Kiba leo akiwa nchini Afrika Kusini amesaini mkataba mkubwa na kampuni ya SONY MUSIC ambayo pia inafanya kazi na wasanii wakubwa kama Chris Brown, Davido na John Legend.
Kiba aliyeachia wimbo wake mpya 'Aje' aliondoka jana kuelekea 'Bondeni' kwa Jacob Zuma na leo ameweka historia mpya kwenye tasnia ya muziki Tanzania.
Msanii huyo sasa atafanya kazi chini ya usimamizi wa kampuni hiyo kubwa ambayo imeshawasaidia wanamuziki mbalimbali duniani kutambulika