HANSPOPPE AWASHANGAA WANAOWAVAMIA VIONGOZI SIMBA

Na Juma JR, DAR ES SALAAM

Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Hans Poppe amewashangaa watu ambao wamekuwa wakijitokeza kuwavamia au kuwalaumu viongozi wa Simba ambao wanatoa kila kitu kadiri ya uwezo wao kuhakikisha timu inafanya vizuri.

Kama hiyo haitoshi, Hans Poppe amesema, beki Hassan Kessy ambaye ameondoka Simba na kujiunga Yanga, waziwazi aliwasaliti.

“Viongozi hawachezi pale uwanjani, kawaida wanafanya kila kitu kuhakikisha wachezaji wanapata na kwenda kucheza.

“Wao ndiyo wanatakiwa kuwa na moyo na klabu, wawe na huruma na mashabiki. Lakini si mtu anapewa kadi nyekundu kwa makusudi kabisa, halafu ,mashabiki wanavamia viongozi.

“Wakati mwingine nanyama kwa kuwa ukibishana na wajinga na wewe utaonekana ni mjinga. Lakini angalia alichokifanya Kessy, kadi nyekundu katika mechi dhidi ya Toto ambayo inaonyesha huyu alipania kuipata.

“Siku chache baadaye anajiunga na timu nyingine, tena kukiwa na tetesi nyingi kuhusiana na ushiriki wake nao. Sasa unataka nini tena uone kama wewe ni shabiki ili kujua tatizo liko kwa nani?” alihoji.

Hans Poppe amesisitiza msimu ujao, wanalazimika kuwa makini sana ili kuepuka wachezaji ambao wanaingia Simba kwa lengo la usaliti.

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA