NGOMA AIPASUA KICHWA YANGA
Na Salum Fikiri Jr, DAR ES SALAAM
MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa mabingwa wa soka Tanzania bara Yanga SC Donald Ndombo Ngoma raia wa Zimbabwe anaipasua kichwa klabu hiyo baada ya kugoma kuongeza mkataba mwingine.
Ngoma amekataa kuongeza mkataba mwingine hasa baada ya kugundua kuwa Yangs hawako tayari kumuuza, Ngoma alitakiwa nchini Australia lakini Yanga waliikalia ofa hiyo.
Na sasa anatakiwa nchini Afrika Kusini lakini pia klabu yake haionyeshi nia yoyote ya kufanya mazungumzo na timu hiyo, hivyo ameamua kutoongeza mkataba ili huu wa sasa unaotarajia kumakizika mwakani uwe wa mwisho kwake.
Ngoma alitua Yanga kwa mkataba wa miaka miwili akitokea FC Platinum ya Zimbabwe na hadi amekuwa tegemeo katika kikosi hicho chs Yanga, Naye msemaji wa Yanga Jerry Muro amezikana taarifa hizo na kudai hakuna klabu yoyote iliyotuma ofa Yanga ya kumuhitaji mshambuliaji huyo