BAKHRESSA AMPELEKA BURE FARID TENNERIFE
Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
MKURUGENZI wa timu ya Azam Fc ya Dar es Salaam Yussuf Said Salim Bakhressa aneamua kumpeleka bure winga wake Farid Mussa Marik hasa baada ya kufaulu majaribio yake katika timu ya Tennerife ya Hispania.
Farid alikwenda kufanya majaribio kwenye timu hiyo inayoshiriki ligi Daraja la kwanza maarufu Sagunda Division na kufaulu lakini timu hiyo imeitangazia Azam dau dogo ikitaka kumnunua.
Lakini bosi huyo ambaye pia ni Wakala wa kimataifa anayetambuliwa na Shirikisho la mpira wa miguu duniani FIFA, Bakhressa ameona ni bora amruhusu kinda huyo kujiunga bure na Tennerife na baadaye akitakiwa na timu nyingine Azam itanufaika