KISA YANGA, TFF YAICHOMOLEA CECAFA KUANDAA KAGAME DAR

Na Prince Hoza, DAR ES SALAAM

SHIRIKISHO la mpira wa miguu nchini TFF limeikatalia Baraza la vyama Afrika mashariki CECAFA kuwa mwenyeji wa michuano ya kombe la Kagame iliyopangwa kufanyika Dar es Salaam.

Rais wa Shirikisho hilo Jamal Malinzi amesema TFF haiwezi kukubali Tanzania iwe mwenyeji wa michuano hiyo kwavile imebanwa na ratiba ya michuano ya kimataifa, Tanzania itakuwa mwenyeji wa michuano ya CAF ambapo klabu ya Yanga itakuwa ikishiriki.

Yanga imeingia hatua ya makundi kombe la Shirikisho barani Afrika hivyo haitaweza kushiriki michuano ya Kagame iliyopangwa kuanza Julai mwaka huu wakati Yanga itakuwa kwenye Shirikisho.

Kwa maana hiyo Yanga haitashiriki Kagame kwakuwa itakuwa sambamba na kombe la Shirikisho, Malinzi amedai kama Yanga haishiriki Kagame haitakuwa na maana kwani Yanga ina mashabiki wengi wanaoingia uwanjani hivyo kuna uwezekano kutopatikana kwa mapato, TFF imelitaka CECAFA kutafuta nchi nyingine kuandaa fainali hizo

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA