STAA WETU: ABDUL 'NAJ' MACHELA, MTOTO WA MCHEZAJI WA SIMBA ANAYETAMANI KUCHEZA VPL
Na Salum Fikiri Jr, DAR ES SALAAM
WAHENGA wanasema mtoto wa nyoka ni nyoka, Mshambuliaji wa zamani wa Simba katika miaka ya 90 akisifika kwa kupiga mashuti makali langoni kwa wapinzani wao, Ali Machela ndiye ninayemwelezea.
Lakini mpachika mabao huyo hatunaye duniani lakini ametuachia mtoto wake ambaye naye amefuata nyayo zake, Abdul 'Naj' Machela ndiye mtoto wa straika huyo wa zamani wa Simba SC.
Naj kama mwenyewe anavyooenda kujiita, ni mmoja kati ya wachezaji wenye vipaji vya hali ya juu, ingawa anajiona kama hana bahati ya kusajiliwa na vilabu vya ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara (VPL).
Mwenyewe anajiona kama ana mikosi ya kupata timu kubwa na ameiambia Mambo Uwanjani kwamba anaumia sana anapoona watoto wa mastaa wa zamani wa Simba au Yanga na timu nyingine kubwa wanasajiliwa na vilabu vya ligi kuu huku yeye akiendelea kusota mchangani.
'Kwakweli sijisikii vizuri wenzangu wanasajiliwa na vilabu kama Yanga, Simba Nk huku mimi nikiendelea kucheza mchangani', anasema Naj ambaye amewahi kuwa mfungaji bora katika mashindano ya mchangani.
Mbali na kubahatika kucheza ligi Daraja la pili huko Zanzibar, lakini Naj anatamani kucheza bara kwani anadai ligi kuu ya bara inalipa kuliko ya visiwani, wapo watoto wa wachezaji wa zamani waliotamba ligi kuu bara ambao kwa sasa wanatikisa.
Mrisho Ngassa anacheza soka la kulipwa Afrika Kusini katika klabu ya Free State Stars, Ngassa ni mtoto wa kiungo wa zamani wa Simba, Pamba ya Mwanza na Taifa Stars Khalfan Ngassa.
Pia wapo wengine kama akina Amiri Maftah, Jeremiah Juma Mgunda, Juma Mahadhi, Waziri Mahadhi, Bakari Mahadhi, Rashid Mahadhi, Habib Mahadhi, wengine ni Salum Abubakar 'Sure Boy', Himid Mao Mkami Hassan Kabunda, Ali Kabunda na wengineo ambao wamerithi mikoba ya wazazi wao.
Naj anazitaka timu zinazoshiriki ligi kuu bara zijitokeze kumsajili kwani anakiwango kizuri ambacho kitakuwa msaada kwao, nyota huyo anayecheza nafasi ya ushambuliaji amewaomba Simba SC kumpa nafasi ili aweze kuonyesha yale aliyokuwa akiyafanya marehemu baba yake mzazi Ali Machela.
Endapo ndoto zake zitatimia, Naj ataungana na nyota hao ambao ni watoto wa wachezaji wa zamani waliotamba ligi kuu bara, Naj aliyeichezea timu ya nyumbani kwao ya Kongowe FC ya Mbagala Dar es Salaam yuko tayari kucheza timu yoyote ili mradi iwe ya ligi kuu au daraja la kwanza.
Lakini msimu ujao mchezaji huyo mwenye mashuti anaweza kuonekana kwenye ligi zetu kubwa hapa nchini, Abdul Naj Machela anaamini kama atakuwa amepewa nafasi basi atawaonyesha vitu vyake