SIMBA YAMBEBA KIBADENI, YADUNDWA 2-1 TAIFA
Na Salum Fikiri Jr, DAR ES SALAAM
SIMBA SC jioni ya leo imeendeleza machungu kwa mashabiki wake hasa baada ya kuduwazwa mabao 2-1 na vijana wa Abdallah Kibadenj JKT Ruvu Uwanja wa Taifa Dar es Salaam mchezo wa mwisho wa ligi kuu bara.
Vijana wa JKT Ruvu ndio walioanza kulisakama lango la Simba lakini mabeki wa timu hiyo walikuwa makini, mabao ya JKT Ruvu yamewekwa kimiani na Abdul Omari yote akifunga kipindi cha kwanza.
Simba waliamka kipindi cha pili wakipata bao la kufuatia machozi lililofungwa na nahodha wake Mussa Hassan Mgosi, KATIKA mchezo mwingine uliofanyika uwanja wa Azam Complex Chamazi, Azam imeifunga 1-0 Mgambo JKT na kuishusha daraja.
Azam sasa amekamata nafasi ya pili ikiiacha nyuma Simba Sc iliyokamata nafasi ya tatu