MOURINHO ATUA MAN UNITED AMWAGA WINO KUKINOA KIKOSI
JOSE Mourinho amesaini kandarasi ya miaka miwili kujiunga na 'Mashetani Wekundu' wa Old Trafford Manchester United na kuondoa uvumi uliozagaa kwa muda mrefu juu ya kujiunga kwake na mashetani hao.
Mourinho kocha mbwatukaji mwenye rekodi za kutisha sasa anakuwa meneja mpya wa Man U timu iliyopoteza heshima yake mara baada ya kuondoka kwa Alex Ferguson maarufu kama Fergie.
Meneja huyo atakuwa na kazi ya kurejesha mataji kama yale ya primia na UEFA Champion League, Mourinho anarithi mikoba ya Lous Van Gaal aliyetimuliwa juma lililopita licha ya kuibebesha taji la FA Cup