BARTHEZ AINUSURU YANGA KULALA MBELE YA MAJIMAJI
Na Exipedito Mataruma, SONGEA
MABINGWA wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara Yanga Sc jioni ya leo imenusurika kichapo mbele ya Majimaji ya Songea Uwanja wa Majimaji mkoani Ruvuma baada ya kutoka sare ya 2-2 mchezo wa ligi kuu bara.
Yanga imefikisha pointi 73 ambazo hazikuweza hata kusogelewa na timu yoyote, Yanga ilikuwa ya kwanza kupata bao la kuongoza lililofungwa na Poul Nonga, Majimaji walisawazisha kupitia Alex Kondo yote yamefungwa kipindi cha kwanza.
Kipindi cha pili Majimaji walilisakama lango la Yanga kama nyuki na kufanikiwa kupata bao la pili lililofungwa na Said Mrisho, Yanga walisawazisha bao kwa njia ya penalti likifungwa na kipa wake Ali Mustafa 'Barthez', goli hilo limeinusuru Yanga kwani ingeweza kulala na kuharibu cv yake