TFF YAMWANGUKIA CANNAVARO
Na Ikram Khamees, DAR ES SALAAM
RAIS wa Shirikisho la mpira wa miguu nchini TFF Jamal Emily Malinzi amemtaka Nahodha na mlinzi wa mabingwa wa ligi kuu bara, Ngao ya Jamii na FA Cup Yanga Sc Nadir Ali Haroub 'Cannavaro' kukubali arejee kwenye timu ya taifa, Taifa Stars.
Cannavaro amekataa kujiunga na kikosi hicho hasa baada ya mwalimu wa timu hiyo Charles Boniface Mkwassa kumvua ubahodha kimafia, awali Cannavaro alikuwa nahodha wa Stars lakini kocha huyo akamvua kimafia na kumvika kitambaa cha unahodha mshambuliaji wa Genk Mbwana Samatta.
Kitendo hicho kilionekana kumuudhi Cannavaro na siku chache ya baadaye akatangaza kujiuzuru kuichezea Stars, lakini Mkwassa ambaye pia alikuwa kocha msaidizi wa Yanga akamteua tena kwenye kikosi chake kinachojiandaa kucheza mechi ya kirafiki na Harambee Stars.
Beki huyo wa kati mwenye mafanikio katika klabu yake ya Yanga amekataa kujiunga na Stars, jana katika mchezo wa fainali kombe la Azam Sports Federation Cup maarufu FA Cup Uwanja wa Taifa Dar es Salaam kati ya Yanga na Azam Rais wa TFF Jamal Malinzi alitumia mwanya huo kuteta na beki huyo na kumuombea msamaha ili arejee kundini