KIIZA ALIA KUNYIMWA UFUNGAJI BORA
Na Salum Fikiri Jr, DAR ES SALAAM
MSHAMBULIAJI wa Simba raia wa Uganda Hamisi Friday Kiiza amesikitishwa na kitendo cha Shirikisho la mpira wa miguu nchini TFF kumnyima tuzo ya ufungaji bora na kumpa Atupele Green Jackson wa Ndanda FC.
Akizungumza a mtandao huu, Kiiza amesema yeye ndiye mfungaji bora wa kombe la Azam Sports Federation Cup maarufu FA Cup kwani amefunga jumla ya magoli matano.
Lakini anashangaa jana Shirikisho hilo limemtangaza Atupele Green wa Ndanda kuwa mfungaji bora wa michuano hiyo wakati si kweli, Kiiza amefunga magoli mawili dhidi ya Burkina Faso ya Morogoro Simba ikishinda mabao 3-0 pia alifunga tena mawili dhidi ya Singida United Simba ikishinda 5-0 na alifunga bao moja dhidi ya Coastal Union, Simba ikilala 2-1.
Atupele Green amefunga magoli manne lakini akapewa zawadi ya ufungaji bora, pia Kiiza anailaumu klabu yake kwakushindwa kumpanga kwenye mechi za mwishoni za ligi kwani anaaminj angemvuka Amissi Tambwe aliyeibuka mfungaji bora