YANGA SASA WAAMUA KUMFUATA NGASSA 'SAUZI'

Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM

MABINGWA wa soka nchini Yanga SC wameachana na ziara yao ya nchini Uturuki na sasa wameamua kuelekea nchini Afrika Kusini kwa ajili ya maandalizi yao ya michuano ya kombe la Shirikisho barani Afrika hatua ya makundi Robo fainali.

Uongozi wa Yanga kupitia mwenyekiti wake wa Kamati ya mashindano Issack Chanji wamemua kubadili ratiba yao ya kuelekea Uturuki ambapo ni karibu kabisa na Algeria ambapo watakwenda kukabiliana na MO Bejala ya Algeria mchezo wa kwanza  kombe la Shirikisho.

Yanga imetinga hatua ya makundi kombe la Shirikisho barani Afrika hivyo italazimika kukutana na timu za MO Bejala ya Algeria, TP Mazembe ya DRC na Medeama ya Ghana.

Kwa maana hiyo Yanga itakuwa imemfuata mshambuliaji wake wa zamani Mrisho Ngassa anayekipiga Free State Stars inayoshiriki Ligi kuu Afrika Kusini

Yanga SC sasa wanakwenda Afrika Kusini

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA