TFF YAPULIZA KIPYENGA UCHAGUZI YANGA
Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
SHIRIKISHO la mpira wa miguu nchini TFF limeutangaza rasmi mchakato wa uchaguzi mkuu wa mabingwa wa bara, Ngao ya Jamii na FA Cup Yanga SC na fomu za kuwania uongozi zikianza kutolewa Mei 27 katika ofisi za Shirikisho hilo uwanja wa Karume Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi ya TFF Wakili Aloyce Komba amesema wanachama wa Yanga wataanza kuchukua fomu za juwa ia uongozi kuanzia Ijumaa Mei 27, Komba amedai taratibu za kulipia ada za uanachama ili kushiriki uchaguzi huo hilo litafanywa na Yanga wenyewe.
Aidha mwenyekiti huyo amedai Yanga wametakiwa kufanya uchaguzi chini ya TFF baada ya kukaidi kufanya wenyewe kwa nuda wa miaka miwili hivyo viongozi wao hawapo kisheria, ameelezea hupatikanaji wa fomu za nafasi ya uenyekiti na makamu wake zitaoatikana kwa shilingi laki mbili na zile za nafasi za ujumbe ni laki moja tu