YANGA NA AZAM HAPATOSHI LEO TAIFA, NI FAINALI YA FA CUP

Na Ikram Khamees, DAR ES SALAAM

KLABU bingwa Afrika mashariki na kati Azam FC jioni ya leo inawavaa mabingwa wa Tanzania bara na wawakilishi pekee wa mashindano ya kimataifa Yanga SC mchezo wa fainali kombe la Shirikisho maarufu FA Cup uwanja wa Taifa Dar es Salaam.

Miamba hiyo kila inapokutana hukamiana sana na mwisho humaliza dakika tisini kwa mwendo wa sare hatimaye kupigiana penalti, mara ya mwisho kukutana kwenye mchezo wa mashindano ya mtoano timu hizo zilifungana kwa zamu.

Katika mchezo wa Robo fainali kombe la Kagame uliofanyika uwanja wa Taifa mwaka jana, Azam ilishinda kwa matuta baada ya sare ndani ya dakika tisini, pia Yanga ikalipiza kisasi katika mchezo wa Ngao ya Hisani kwa mikwaju ya penalti.

Pambano la leo litakuwa gumu hasa kutokana na vikosi vya timu zote kuimarika, Yanga ikiwa na hamasa ya kutinga hatua ya makundi kombe la Shirikisho barani Afrika pamoja na kutwaa ubingwa wa bara, Azam itataka kuwahakikishi mashabiki wake kwamba walistahili ubingwa wa Kagame, Ngoja tuone

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA