YANGA YAWAFUNGA MIAKA MITATU BARTHEZ, YONDANI NA OSCAR JOSHUA, SIMBA MPOO
Na Saida Salum, DAR ES SALAAM
MABINGWA wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara, Ngao ya Jamii na FA Cup, Yanga SC leo imewaongeza mikataba mipya nyota wake watatu Oscar Joshua, Ali Mustapha 'Barthez' na Kevin Yondani.
Wachezaji hao kila mmoja wamesainishwa mkataba wa miaka mitatu kwa maana hiyo wataendelea kukipiga na Yanga hadi mwaka 2019, Barthez alikuwa akitajwa katika usajili wa Simba SC pamoja na kiungo Salum Telela.
Yanga imeamua kuwapa mikataba mirefu nyota hao hasa kutokana na msaada wao mkubwa waliouonyesa msimu huu wakifanikisha mataji matatu makubwa yaliyo chini ya Shirikisho la mpira wa miguu nchini TFF.
Vilevile wachezaji hao wameisaidia Yanga kufuzu kwa mara ya kwanza na kuandika historia kuwa klabu ya kwanza nchini na Afrika mashariki kwa ujumla kuingia hatua ya makundi konbe la Shirikisho barani Afrika