BABA MANYIKA AMKATIA TAMAA MWANAYE

Na Prince Hoza, DAR ES SALAAM

BABA wa kipa wa Simba Sc Manyika Peter Manyika amemkatia tamaa mwanaye Peter Manyika kwa madai hawezi kurejea tena kwenye makali yake kwa sababu alishindwa kuzingatia maagizo yake.

Akizungumza na Mambo Uwanjani hivi karibuni, Manyika amesema, mwanaye ameshindwa kuzingatia maagizo yake kwani alilewa penzi la Video Queen wa bongofleva.

Manyika aliyewahi kuitwa Tanzania One amedai mwanaye huyo hawezi tena kuitwa Tanzania One kama alivyokuwa yeye hapo zamani kwavile hakuzingatia mafundisho yake, Manyika ameanzisha chuo chake cha kuwanoa makipa mbalimbali akiwemo mwanaye lakini anashangaa anashuka kiwango kila kukicha.

Kipa huyo aliyewahi kutamba akiwa na Mtibwa Sugar, Sigara, Yanga Sc na Taifa Stars, amesikitishwa na kiwango cha mwanaye ambaye kwa sasa anatumika kama kipa wa akiba wakati hapo mwanzo aliaminika langoni akianza kama kipa chaguo la kwanza

Peter Manyika wa Simba anadaiwa kushuka kiwango

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA