MICHANO: P- FUNKY MAJANI, DHARAU ZIMEMPOTEZA KWENYE MUZIKI

Na Mkola Man, TANGA

YAP......yap.....yap....leo Michano inamchana prodyuza P Funky Majani ambaye anamchango mkubwa sana katika tasnia ya muziki wa kizazi kipya hapa nchini Tanzania mastaa wote unaowajua walitoka kwake, kiufupi uwezi kuuelezea muziki wa hapa bongo bila kumtaja.

Jina lake halisi ni Poul Mathiyas Khalfan ni chotala, ila dharau na kujiamini ndio chanzo cha anguko lake lililosababisha samaki aliowabeba waoze kisha akashindwa kustahimili changamoto baada ya Media kumkwamisha kwa kumvalisha miwani meusi gizani ili asione.

Miwani hiyo yenye kiza ilimfanya ashindwe kuona mbele pale alipobadilisha mfumo wa muziki na kuwapa nafasi maprodyuza wengine waliokuwa hawajulikani na kuwapa nafasi kubwa kama wanaweza pasipo kuweza ikawapa moyo na uzoefu kwakuwa P Funky alikuwa anadili na mastaa tu pasipo wasanii wachanga.

Na watu walikuwa wanataka ladha mpya nadhani akujua muziki ni kama biashara uwezi kuwabagua wateja, huyu ananunua sigara mwingine sukari mwisho wa siku wote ni wateja, Yaap Tukutane wiki ijayo mimi Mkola Man Mwanatanga ciao

P Funky Majani amepotea kutokana na dharau zake

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA