SIMBA NA JKT RUVU NI KUSUKA AU KUNYOA, YANGA NA MAJIMAJI NGOMA INOGILE

Na Prince Hoza, DAR ES SALAAM

LIGI kuu ya Vodacom Tanzania bara inafikia hatamu leo kwa vilabu vyote  vinavyoshiriki ligi hiyo, tayari mabingwa wa ligi hiyo wameshajulikana ni Yanga Sc na vita pekee imehamia kusaka mshindi wa pili na zitakazoshuka daraja.

Ligi hiyo inaendelea leo lakini mechi zinazosubiriwa kwa hamu ni tatu ti zitakazoshirikisha vigogo vya soka hapa nchini, Uwanja wa Taifa Dar es Salaam Simba Sc wanaikaribisha JKT Ruvu wakati pale Chamazi Azam Fc wataialika JKT Mgambo ya Handeni Tanga.

Pambano lingine kali litakuwa mjini Songea kati ya mabingwa wa ligi hiyo Yanga Sc na wenyeji Majimaji ya Songea, uhondo wa ligi hiyo upo kwenye nafasi ya pili kati ya Simba na Azam.

Azam inashika nafasi ya pili na pointi 63 wakati Simba ina pointi 62 zote zikiwa zimecheza mechi 29 na leo itajulikana nani atashika nafasi ya pili, pia vita itakuwepo katika janga la kushuka daraja ambapo tayari timu ya Coastal Union imeshashuka daraja, vita hiyo sasa ipo kwa timu mbili zitazoungana na Coastal

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA