YANGA WATAMBA KUILIPIA SIMBA DENI LA MOSOTI FIFA
Na Salum Fikiri Jr, DAR ES SALAAM
YANGA SC wametamba kuilipia Simba Sc deni lake inalodaiwa na mchezaji wake wa zamani Mkenya Donald Mosoti aliyeshinda kesi FIFA na kutakiwa alipwe shilingi Mil 64 ama sivyo FIFA wataishusha daraja timu hiyo kongwe.
Mkuu wa kitengo cha Habari na Mawasiliano wa Yanga Sc Jerry Muro amesema Yanga hawako tayari kuiona Simba ikishushwa daraja kwani soka la Tanzania litaporomoka.
Akizungumza kwa hisia, Muro amedai hatanii ni ukweli kwamba watawalipia deni hilo kwani kuna uwezekano mkubwa Yanga ikakosa kushiriki hatua ya makundi kombe la Shirikisho Afrika iwapo FIFA itaifungia Tanzania kutokana na kosa la Simba