HATIMAYE ZILE T: SHIRT ZA KIJANJA ZINAPATIKANA MADUKANI
Na Saida Salum, DAR ES SALAAM
HATIMAYE zile tisheti za kijanja zilizobuniwa na mbunifu chipukizi wa mavazi Ndulumo Junior Mbazi zimeanza kusambazwa madukani hapa jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na Mtandao huu, Ndulumo Junior amesema tayari tisheti zake zenye maneno mbalimbali ya kufurahisha yakiwemo 'UsI4c Nikuamini' zimeanza kusambazwa madukani.
Tisheti hizo zinapatikana katika maduka kadhaa Kariakoo na nyingine zipo Tabata Da West kwenye saluni ya kike ya mwanadada Veronica Mdamo na pia katika stationary ya Salma iliyopo Tabata Mtambani karibu na kwa mzee Njalangi.
Waweza pia kumpigia simu yake 0713690868