YANGA YATINGA ROBO FAINALI AFRIKA, DIDA AWA SHUJAA

Na Exipedito Mataruma, ANGOLA

YANGA SC ya Tanzania jioni ya leo imefanikiwa kuingia Robo fainali ya kombe la Shirikisho baranj Afrika licha ya kulala 1-0 na wenyeji wao GD Sagrada Esparanca ya Angola mchezo uliokuwa na figisu nyingi uliofanyika Dundo Angola.

Esparanca wakitumia vema uwanja wao wa nyumbani wakibebwa na mwamuzi wa mchezo ikishuhudiwa wachezaji watano wa Yanga wakionyeshwa kadi za njano na mwingine nyekundu.

Beki na nahodha wa Yanga Nadir Haroub Cannavaro alipewa kadi nyekundu, kipa wa Yanga Deo Munishi 'Dida' alicheza vizuri na kuibuka shujaa, Yanga waliruhusu bao kipindi cha kwanza na ilionekana dhahili kama wangepoteza mchezo huo.

Eaparanca walipewa penalti zikiwa dakika za lala salama lakini Dida akafanikiwa kupangua mpira huo, Kwa maana hiyo Yanga sasa imefuzu Robo fainali itakayochezwa kwa mtindo wa makundi, HONGERA YANGA SC

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA