MASHUJAA YANGA KUWASILI KESHO SAA 8 MCHANA, KUINGIA KAMBINI KUWAVAA MAJIMAJI
Na Exipedito Mataruma, DUNDO
MASHUJAA wa Tanzania Yanga Sc walioweka historia jana ya kuwa timu ya kwanza nchini na ukanda mzima wa Afrika mashariki na kati kutinga hatua ya makundi kombe la Shirikisho barani Afrika baada ya kuiondosha GD Sagrada Esparanca ya Angola kwa jumla ya mabao 2-1.
Yanga jana ilifungwa bao 1-0 katika uwanja wa Esparanca mjini Dundo Angola, licha ya kipigo hicho Yanga imefuzu hatua ya makundi baada ya kutangulia kushinda mabao 2-0 yaliyofungwa na Simon Msuva na Matteo Antony.
Mabingwa hao wa bara watawasili nchini kesho wakitokea nchini Afrika Kusini ambako nako wamewasili wakitokea Angola, Yanga watatua saa nane mchana lakini moja kwa moja wataingia kambini kujiandaa na mchezo wao wa ligi kuu bara dhidi ya Majimaji utakaopigwa mjini Songea Jumamosi