TAIFA STARS YAISHIKA HARAMBEE STARS
Na Salum Fikiri Jr, NAIROBI
TIMU ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars jioni ya leo imeilazimisha sare ya 1-1 timu ya taifa ya Kenya Harambee Stars mchezo wa kirafiki wa kimataifa uwanja wa Moi Kasarani jijini Nairobi.
Ikicheza kwa kujiamini, Taifa Stars ilikuwa ya kwanza kujipatia bao la uongozi lilikofungwa na mshambuliaji wake Elius Maguli aliyepokea krosi murua ya beki wa pembeni Juma Abdul Mnyamani.
Harambee Stars iliyoonekana kususiwa na mashabiki wake ilijipatia bao la kusawazisha lililofungwa na mshambuliaji wake wa kimataifa anayekipiga Southmpton ya England Victor Wanyama na kuikoa nchi yake kulala mbele ya vijana wa Charles Boniface Mkwassa