REAL MADRID YATWAA UBINGWA WA ULAYA
REAL MADRID mabingwa wa Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya baada ya kuwalaza Atletico Madrid fainali kupitia mikwaju ya penalti. Mkwaju wa ushindi umefungwa na Cristiano Ronaldo. Mechi ilimalizika 1-1 muda wa kawaida na wa ziada.
Real Madrid wanaonolewa na mchezaji wao wa zamani Zinedine Zidane ilikuwa ya kwanza kupata bao lililofungwa Sergio Ramos, licha ya kuingia bao hilo, Real walionekana kuishambulia Atletico.
Kocha wa Atletico Diego Simione alifanya mabadiliko ya kumwingiza Carlossa ambaye ndiye aliyefanikiwa kusawazisha bao hilo na kufanya matokeo yawe 1-1.
Mchezo huo ulimalizika kwa sare na kuelekea kwa dakika za nyongeza ambapo hata hivyo hazikufangana, ndipo mikwaju ya penalti ilipoanza kupigwa na Real kushinda kwa mikwaju 5-3, Ronaldo ndiye aliyefinga bao la ushindi hasa baada ya kipa wake kuokoa penalti ya Atletico