WABABE YANGA WATUA NA DEGE LA SOUTH AFRIKA, MASHABIKI WAFURIKA
Na Exipedito Mataruma, DAR ES SALAAM
YANGA SC imewasili jioni ya leo wakitokea nchini Afrika Kusini ambako nako walitokea Angola walikofanikiwa kutinga hatua ya makundi kombe la Shirikisho barani Afrika.
Msafara wa wachezaji, benchi la ufundi na viongozi wa Yanga ulitua majira ya saa tisa alasiri na kulakiwa na maelfu ya mashabiki wa timu hiyo ambapo msafara huo ulielekea makao makuu ya klabu mtaa wa Jangwani na Twiga Dar es Salaam.
Yanga ilifungwa bao 1-0 na GD Sagrada Esparanca katika mchezo wa marudiano uliofanyika Jumatano iliyopita uwanja wa Esparanca mjini Dundo nchini Angola, Yanga imeitoa Esparanca kwa jumla ya mabao 2-1 baada ya kushinda 2-0 katika mchezo wa kwanza uliopigwa Dar ea Salaam