YANGA YAWAENDEA MO BEJALA UTURUKI
Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
YANGA SC wataweka kambi yao bchini Uturuki katika maandalizi yao hatua ya makundi kombe la Shirikisho barani Afrika dhidi ya Mo Bejala ya Algeria.
Mabingwa hao wa bara, Ngao ya Jamii na kombe la FA, wataondoka nchini mara baada ya kumalizika kwa likizo kwa wachezaji wake ya siku tano ambapo wachezaji wake wengine wamejiunga na timu za taifa.
Haruna Niyonzima (Rwanda), Vincent Bossou (Togo), Deo Munishi, Mwinyi Hajji, Deus Kaseke na Juma Abdul (Tanzania), wachezaji hao wataungana na wenzao wengine kuanza safari ya Uturuki.
Kamati ya mashindano ya Yanga Sc imeketi na kocha mkuu wa mabingwa hao Mholanzi Hans Van der Pluijm kuzungumzia kambi ndipo Mholanzi huyo alipoichagua Uturuki kama sehemu sahihi kwa kujiandaa na Waalgeria hao.
Hii ni mara ya tatu kwa Yanga Sc kwenda nchini Uturuki kuweka kambi, Yanga imefuzu hatua ya makundi kombe la Shirikisho barani Afrika na itacheza na timu za TP Mazembe, Madeama na Mo Bejala