JUMA ABDUL AWA MCHEZAJI BORA WA MWEZI APRILI
Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
BEKI wa kulia mwenye mambo adimu wa Yanga Sc Juma Abdul Jaffari Mnyamani leo ametangazwa na Shirikisho la mpira wa miguu nchini TFF kuwa mchezaji bora wa mwezi Aprili baada ya kuwashinda wenzake.
Abdul sasa atajinyakulia kitita cha Vodacom shilingi Mil moja, beki huyo amekuwa bora hasa baada ya kuonyesha kiwango kikubwa ndani ya mwezi Aprili kuisaidia Yanga kutwaa ubingwa wa bara.
Beki huyo aliyesajiliwa misimu miwili iliyopita akitokea Mtibwa Sugar ya Morigoro amekuwa katika kiwango kizuri na kumfanya kocha mkuu wa timu ya taifa Charles Boniface Mkwassa kumjumuhisha kwenye kikosi chake