BMT, TFF MNATAKA KUIPELEKA WAPI YANGA?
Na Prince Hoza, DAR ES SALAAM
BARAZA la Michezo la Taifa (BMT) lilipokea agizo kutoka Wizara ya Habari, Michezo, Utamaduni na Wasanii la kutaka vyama vyote vya michezo na vilabu ambavyo havijafanya uchaguzi vifanye haraka ifikapo Juni mwaka huu.
Waziri wa wizara hiyo Nape Moses Nnauye alikuwa mstari wa mbele kuvitaka vilabu na vyama kuchaguana kwa njia ya kidemokraisa, BMT ililigeukia Shirikisho la mpira wa miguu nchini TFF na kulitaka liwaambie wanachama wao ambao hawajafanya uchaguzi wafanye haraka mwaka huu.
Yanga SC ikakutwa na hatia kwani haijafanya uchaguzi wake kisheria tangu mwaka 2014 ambapo muda wa uongozi wao ulifikia tamati, hata hivyo wanachama wa klabu hiyo walimuongezea muda zaidi nwenyekiti wao Yusuf Mehbood Manji kwa kipindi cha mwaka mmoja.
Manji aliendelea kukaa madarakani kwa mwaka mmoja zaidi na makubaliano yao wafanye uchaguzi mwaka jana 2015, lakini nao pia hawakufanya tena uchaguzi na kisingizio kikubwa ni uchaguzi mkuu wa nchi ambao ulifanyika Oktoba 25, 2015.
Safari hii sasa TFF imeikomalia Yanga kufanya uchaguzi huo lakini kwa masharti magumu mno, TFF imeanzisha mchakato huo kwa kuwataka Wanayanga kuchukua fomu za kuwania nafasi mbalimbali kwenye Shirikisho hilo.
Kamati ya uchaguzi huo ni ya TFF ikishirikiana na sekretalieti ya Yanga kwa ajili ya kuwatambua Wanayanga, lakini Kamati hiyo ya TFF inataka kutumia katiba Yanga ya mwaka 2010 huku pia ikiwazuia wanachama wa Yanga wenye kadi mpya za ATM hawataruhusiwa kupiga kura.
Yanga wanayo kamati yao ya uchaguzi inayoongozwa na Sam Mapande ambayo pia ikisimamia mchakato huo, kitendo cha Yanga kunyimwa haki ya kusimamia uchaguzi huo kungepelekea utaratibu wa kufanyika uchaguzi huo.
Yanga wangehitisha mkutano mkuu wa wanachama na wangeamua wenyewe watumie katiba ipi, kuna uwezekano mkubwa baadhi ya Wanayanga wenye mapenzi na klabu yao, pia kuna athali Yanga wakapata viongozi wasiokuwa na mapenzj na timu yao.
Miaka ya nyuma Yanga walikuwa na viongozi wao ambao kila kukicha mwenendo wa timu yao haukuwa mzuri, mitaa ya Jangwani na Twiga bakora zilitapakaa mpaka FFU walitumika kutuliza ghasia, Lakini kwa sasa Yanga wanafurahia timu yao kiasi kwamba hata mahasimu wao Simba wanaona donge.
Yanga ikiwa chini ya mwenyekiti wake Bilionea Yusuf Mehbood Manji imefanya mambo mengj ya maana ikiwemo kuhudumia wachezaji wake vizuri, Yanga imetwaa ubingwa wa bara mara mbili mfululizo, Ngao ya Jamii mara mbili mfululizo na kombe la FA, pia Yanga imetinga hatua ya makundi kombe la Shirikisho barani Afrika.
Yanga hiyo hiyo imeweza kumtambia mtani wake Simba Sc kwa kumfunga mara mbili mfululizo, Yanga iliifunga Simba mabao 2-0 kila mechi za Ligi kuu bara.
Wakati Yanga ikiwa inafanya vizuri lakini viongozi wake sidhani kama wana kadi za zamani kama inavyotaka TFF, kwa maana hiyo kuna uwezekano mkubwa Yanga ikapotea kwa staili hiyo, TFF wanaweza kuifanya Yanga iongozwe na mamluki ambao watatumia mwanya huo.
Sifurahishwi na uchaguzi wa Yanga unaosimamiwa na TFF, inafahamika waziwazi kwamba Yanga inajiendesha yenyewe hivyo inapaswa kuamua hatma yake yenyewe, mimi si mwanachama wala mpenzi wa Yanga lakini siungi mkono unafiki huu wa TFF na BMT ambao wanataka kuipeleka Yanga huko kusikojulikana
Mwandishi wa makala hii anapatikana kwa namba 0652626627