LVG AFUNGASHIWA VIRAGO MAN UNITED
KLABU ya Manchester United ya England imetangaza kumfuta kazi meneja wake Lous Van Gaal (LVG) licha ya kufanikiwa kuibebesha taji la FA Cup mwishoni mwa juma lililopita.
Van Gaal ameondoshwa kwenye kikosi hicho hasa baada ya kushindwa kuipa taji la primia na kujikuta ikiangukia nafasi ya tano, Man United imepoteza makali yake tangia alipoondoka Babu Alex Ferguson.
Kocha huyo Mdachi alichukua mikoba ya Mskochi David Moyes ambaye naye alifurushwa hasa kufuatia kufanya vibaya kwa klabu hiyo kongwe, tayari Man United imethibitisha kutua kwa kocha mbwatukaji Jose Mourinho ambaye amewahi kuzinoa Porto, Chelsea, Inter Milan na Real Madrid