NGASSA AITUMIA SALAMU ZA PONGEZI YANGA
MSHAMBULIAJI wa kimataifa raia wa Tanzanja anayekipiga Free State Stars inayoshiriki Ligj kuu ya ABSA ya nchini Afrika Kusini Mrisho Ngassa ameitumia salamu za pongezi Yanga Sc kwa kufanikiwa kuingia hatua ya makundi kombe la Shirikisho barani Afrika.
Akizungumza na Mambo Uwanjani kutoka Afrika Kusini, Ngassa aliyewahi kuzichezea Yanga Sc Simba na Azam amedai hatua iliyofikia Yanga ni ya kupongezwa.
Yanga jana ilifungwa bao 1-0 na GD Sagrada Esparanca ya Angola lakini ikafuzu kwenda kwenye hatua ya makundi hasa baada ya kushinda 2-0 mjini Dar es Salaam