TSHABALALA AWA MCHEZAJI BORA WA SIMBA APRILI
Na Mrisho Hassan, DAR ES SALAAM
BEKI wa kushoto wa Simba Sc Mohamed Hussein 'Tshabalala' amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa klabu ya Simba wa mwezi Machi na Aprili mwaka huu imeelezwa.
Kupitia mtandao wa Simba Sc Tanzania, Tshabalala amechaguliwa kuwa mchezaji bora baada ya kutoa msaada mkubwa ndani ya klabu hiyo iliyomaliza kwenye nafasi ya tatu ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara.
Tshabalala ambaye pia ni mchezaji wa timu ya taifa, Taifa Stars amekuwa katika kiwango kizuri siku za hivi karibuni na kuwashangaza watu mbalimbali wanaofuatilia mchezo huo