DANGOTE KUIMWAGIA MAPESA NDANDA FC
Na Saida Salum, MTWARA
BILIONEA Aliko Dangote raia wa Nigeria anatajwa kuwekeza kwenye timu ya ligi kuu ya Ndanda Fc ya mjini hapa, endapo bilionea huyo namba moja barani Afrika atawekeza kwenye timu hiyo basi tutegemee mabadiliko makubwa.
Habari ambazo bado hazijathibitishwa zinasema bilionea huyo mwenye viwanda vya kutengeneza Cement ya aina yake ya Dangote inayouzwa kwa gharama nafuu.
Bilionea anatajwa kuichukua timu hiyo kama mdhamini hivyo kutawafanya Ndanda kuogelea manoti, hii ni mara ya pili kwa Ndanda kupata wafadhili kwani tayari ilishaonja noti za mfanyabiashara wa matairi Nassoro Binslum ambaye hata hivyo ameachana na Ndanda