DIAMOND AZIDI KUPAA KIMATAIFA, ATAJWA TUZO ZA BET

Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM

MSANII wa muziki wa kizazi kipya maarufu bongofleva Naseeb Abdul ama Diamond Platinumz ametajwa kuwania tuzo mashuhuri nchini Marekani za BET ambazo zinajumuhisha wanamuziki maarufu duniani kote.

Diamond ametangazwa kuwa miongoni mwa wanamuziki mashuhuri ukanda wa Afrika mashariki kuwania tuzo hizo ikiwa ni mara ya pili tangia alipoteuliwa mwaka jana.

Msanii huyo mwenye rekodi ya kutwaa tuzo mbalimbali amekuwa pekee katika ukanda huu kuwania tuzo hizo, Diamond sasa atakula sahani moja na mastaa mbalimbali duniani kama Rihhana, Drake, P-Diddy, 50 Cent na wengineo ambao ni wasanii wakubwa

Diamond Platinumz ametajwa kwenye tuzo za BET

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA