MICHANO: BELLE 9 NI KAMA MWANARIADHA MWENYE NGILIMAJI
Na Mkola Man, TANGA
YAP.....yap.....yap...Michano leo inamchana Belle 9 Mruguru asiye na bahati ama asiye na mipango ya ushindi kila anaposhiriki kwenye tuzo uangukia pua.
Ingawa anauwezo wa kushinda kabisa ila hushindwa japo nyimbo zake ni nzuri kuliko anaoshindana nao.
Baadhi ya nyimbo zake ni kama vile 'Sumu ya penzi', 'Masogange'. 'Amerudi', 'Ladha' na nyinginezo, pia amekuwa daraja kwa wasanii waliopata mafanikio.
Ninachoamini mimi bado ajajua maana ya mashindano ama anajiamini sana, dunia ya leo kila unachokiona kizuri ujuwe kimetangazwa kupitia vyombo vya habari, siyo Tv na redio peke yake kama anavyofanya yeye.
Belle 9 ni kama mwanariadha anayekimbia akiwa na ngilimaji kiufupi hawezi kushinda, Michano inamshauri abadilike kwani mashabiki wake wanatamani ushindi wake.
Tukutane Wiki ijayo kwenye Michano ya Mkola Man Mwanatanga