NDULUNO JUNIOR AIBUKA NA T:SHIRT ZA KIJANJA
Na Prince Hoza, DAR ES SALAAM
MBUNIFU wa mavazi anayechipukia hapa nchini Ndulumo Junior ameibuka na mavazi ya kijanja yawafaayo vijana wa kileo ambayo ni T;Shirt za rangi mchanganyiko na tayari zimeingia sokoni.
Akizungumza leo na Mambo Uwanjani, Ndulumo Junior amesema ameamua kuwa mbunifu wa mavazi na ujio wake na T:Shirt za kijanja utamfanya akubalike na jamii hasa vijana ambao wameonekana kuzikubali haraka pamba zake.
T:Shirt hizo zenye mchanganyiko wa rangi zimeandikwa 'Usi4C Nikuamini' na zinapatikana madukani, 'Kwa sasa nimezisambaza sehemu mbalimbali ikiwemo kwenye saluni za kike na za kiume pia Stationary na kwingineko', alisema mbunifu huyo anayemiliki duka la nguo Kariakoo jijini Dar es Salaam