Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Februari, 2025

Skudu Makudubela atua AS Vita

Picha
Mchezaji wa Zamani wa Yanga Skudu Makudubela (34) amesajiliwa na klabu ya As Vita club ya Dr Congo. Skudu amesaini mkataba wa miezi nane (8) wenye kipengele cha kuongeza mwaka mmoja(1) mwingine.

Mabilioni ya Waarabu, kumrudisha Feitoto, Yanga

Picha
Klabu ya Young Africans inatajwa itapokea kiasi kikubwa cha fedha watakapofanya biashara ya kuwauza Clement Mzize na Aziz Stephane Ki mwisho wa msimu huu. Kiasi watakachopata wanao uwezo wa kubisha hodi tena pale Chamazi wakamrejesha Feisal Salum halafu wakamsainisha na Djibril Silla ambaye inatajwa amegomea ofa ya mkataba mpya wa kuendelea kusalia Azam Complex.

Clara Luvanga apiga hat trick timu yake ilishinda 7-0

Picha
Nyota wa Tanzania Clara Luvanga ameisaidia timu yake ya Al Nassr FC kupata ushindi wa mabao 7-0 dhidi ya Eastern Flames kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya Saudi Arabia, katika mchezo huo Luvanga amefunga mabao matatu (Hat trick) na kufikisha jumla ya mabao 13

Wakala wa Tshabalala adai timu mbili zinamtaka

Picha
Mlinzi wa kushoto wa klabu ya Simba Mohamed Hussein kupitia kwa wakala wake Carlos Mastermind ameweka wazi kuwa kuna klabu mbili kutoka nje ya nchi zinazoitaka saini ya nyota huyo. " Kuna klabu ya Afrika Kusini imetualika kufanya mazungumzo.Kuna klabu ya Libya imeonyesha kumtaka. Kama uongozi wa mchezaji hatujakaa naye kujua mpango wake ni upi lakini tutakaa, " Carlos Mastermind, Msimamizi wa Nahodha wa Simba Sc Mohamed Hussein 'Tshabalala

Yanga yaishusha kileleni Simba

Picha
Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu bara Yanga SC jioni ya leo imechupa kileleni mwa msimamo wa Ligi hiyo baada ya kuilaza Kagera Sugar ya Bukoba mabao 4-0 katika uwanja wa KMC Complex jijini Dar es Salaam. Kwa matokeo hayo Yanga imefikisha pointi 42 ikicheza mechi 16, ikiishusha Simba yenye pointi 40. Mabao ya Yanga yamefungwa na Clement Mzize dakika 31, Mudathir Yahya dakika ya 60, Pacome Zouzoua (penalti) dakika ya 78 na Kennedy Musonda dakika ya 86. Hata hivyo Stephanie Aziz Ki alikosa penalti ambapo jumla ingekuwa bao 5, kesho Tabora United wataikaribisha Simba uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora