Wenyeji Azam FC wamechomoa goli mbele ya Namungo FC ya kufungana bao 1-1 mchezo wa Ligi Kuu bara uwanja wa Azam Complex uliopo Chamazi.
Namungo FC walikuwa wa kwanza kupata bao dakika ya 10 kupitia kwa Khalid Nyenye kabla ya Gibril Silla dakika ya 42 kuisawazishia Azam FC na kuambulia pointi moja ambazo zitawafanya wafikishe pointi 45 na michezo 22 ikishika nafasi ya tatu nyuma ya Simba.
Namungo FC sasa imefikisha pointi 23 ikishika nafasi ya 14 ikiishusha Pamba Jiji ikiwa imecheza mechi 22.