Mfanyabiashara maarufu na mdau mkubwa wa soka nchini, Azim Dewji amesema hakuna haja ya kutumia gharama kubwa kununua na kutumia vifaa vya VAR, lakini zitumike TV kuangalia marudio ya matukio ili kufanya maamuzi.
Dewji ameyasema hayo leo Jumatano Februari 26, 2025 kupitia mjadala wa Mwananchi X Space wenye Mada isemayo 'Makosa ya waamuzi Ligi Kuu Bara, nini kifanyike'.
"Hakuna haja ya kutafuta VAR, waamuzi wawe wanaangalia marudio ili wajue makosa yao ili kujireke-bisha, hakuna haja ya kuingia gharama wakati TV na VAR hakuna tofauti," amesema.