Yanga yaichabanga bila huruma Mashujaa FC 5-0
Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu bara Yanga SC jioni ya leo imezidi kujikita kileleni mwa msimamo baada ya kuichabanga bila huruma Mashujaa FC mabao 5-0 katika uwanja wa Lake Tanganyika mjini Kigoma.
Kwa ushindi huo Yanga imefikisha pointi 55 ikiwa imecheza mechi 21 ikiwaacha watani zao kwenye nafasi ya pili na pointi 50 wakiwa wamecheza mechi 19.
