Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa ligi Tanzania (TPLB) ,imewapa Onyo kali viongozi wa klabu ya Yanga kufuatia kitendo chao cha kuingia Uwanjani katika eneo la kuchezea (Pitch Area) ,kwenye mchezo kati Ya Yanga na Singida black Stars uliopigwa kwenye Uwanja wa Kmc,Mwenge nakumalizika kwa Yanga kuibuka na ushindi wa magoli 2-1.
Taarifa hiyo iliyotolewa siku ya leo ya ,Februari 23, 2025 na Kamati hiyo kufuatia kikao chake cha Februari 21, 2025 imeeleza kuwa viongozi hao wa klabu ya Yanga walioingia uwanjani walisababisha kukosekana kwa utulivu wakati wa mahojiano ya mdhamini mwenye haki za matangazo ya runinga.