Yanga yaitumia salamu Simba

Pamba Jiji imeshindwa kuutumia vema uwanja wake wa nyumbani wa CCM Kirumba mjini Mwanza baada ya kufungwa mabao 3-0 na mabingwa watetezi wa Ligi hiyo Yanga SC.

Kwa matokeo hayo jahazi la Pamba Jiji inayonolewa na mchezaji wa zamani wa Yanga SC, Fred Minzirp inabaki na pointi zake 22 ikicheza mechi 22 ikiwa nafasi ya 14.

Mabao ya Yanga yamefungwa na Chadrack Isaack Boka dakika ya 28, Stephanie Aziz Ki aliyefunga mawili dakika ya 74 na 76, kesho Simba SC watakuwa ugenini dhidi ya Coastal Union uwanja wa Sheikh Amri Abeid Kaluta jijini Arusha