NI simulizi ya Azam FC na ardhi ya Kondoa, Dodoma! Ni simulizi iliyojificha kuwa mawinga wote wawili wazawa wa Azam wanatokea Kondoa,
Iddi Seleman Nado na Zidane Ally Sereri, ila huyu mtoto Zidaneni imani ya kaka yangu Jeremia Chido pale Dodoma Jiji bila kusahau Academy ya Makole, Dodoma!
Heshima pia kwa baba yangu Fortunatus Johnson ambaye ni CEO wa Dodoma Jiji, walimwamini akiwa mdogo sana.
Kwa mara ya kwanza nilimshuhudia akiwa na UNDER 20 ya Dodoma Jiji, miaka mitatu nyuma nikaamini dogo anaondoka.
Ni staa mpya wa ardhi hii, mchezaji mkubwa wa baadae! Kila la heri Zidane kwa heshima ya mitaa ya Dodoma na ardhi ya Kondoa Nyumbani kwenu.
Goli lake dhidi ya Wekundu wa Msimbazi, Simba SC limezima MIDOMO ya mashabiki wengi wa soka jijini Dar es Salaam na Tanzania kwa ujumla.
Zile tambo za Ahmed Ally sijui zimeishia wapi! Jiji lipo kimya, gumzo ni yeye Zidane Sereli Mrangi wa Kondoa, thank sana dogo.
ASANTENI