Rais wa Yanga aipa msaada wa vifaa Zalan FC
Klabu ya Zalan FC ya Sudan Kusini imetangaza kupokea vifaa walivyoahidiwa na Rais wa Klabu ya Yanga,Eng Hersi Said ikiwa ni mipira, jezi za mechi na mazoezi na viatu rasmi vya michezo yao.
Baada ya kupokea vifaa hivyo, Klabu hiyo imemshukuru Rais wa Klabu ya Yanga kwa moyo wake wa utoaji.




