Mkuu wa mkoa wa Arusha, Paul Makonda amealika timu nne za soka la wanawake kushiriki michuano ya Samia Suluhu Hassan Super Cup 2025 itakayoanza kutimua vymbi Machi 4 hadi 6.
Timu zilizopokea mualiko ni JKT Queens, Fountain Gate Queens, Simba Queens na Yanga Princess.
Timu hizo zitaanza kwa kucheza nusu fainali tarehe 4 na kufuatiwa na fainali tarehe 6.