TFF yamfungia Mourinho


Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini Uturuki (TFF) limemfungia michezo minne na faini zaidi ya Euro 40,000 (40,000£) Kocha wa Fenerbahce, Jose Mourinho kutokana na kauli alizotoa baada ya mchezo wao dhidi ya Galatasaray.

Baada ya mechi ya Jumatatu kumalizika kwa sare ya 0-0, Mourinho mwenye umri wa miaka 62 alisema benchi la ufundi la Galatasaray limekuwa “likiruka kama nyani”.

Pia inasemekana alirudia ukosoaji wake dhidi ya waamuzi wa Uturuki.

Licha ya kauli hizo Klabu ya Fenerbahce imeeleza kuwa kauli hizo za Mourihno zimeeleweka tofauti lakini hazikuwa na maana ya kuonyesha unyanyapaaji.

Siku ya Alhamisi Baraza la Nidhamu la TFF lilitoa adhabu ya kutocheza mechi mbili kutokana na maoni yake dhidi ya mwamuzi wa nne na mechi mbili za nyongeza kutokana na kauli alizozitoa kwenye benchi la Galatasaray.



#WasafiSports