Pyramids yaigomea Getafe kwa straika wake

Unaambiwa Klabu ya Pyramids Katika dirisha dogo la Januari matajiri hao wa Ligi Kuu nchini Misri wamegoma kabisa kumuachia mshambuliaji wao hatari Ibrahim Adel kwenda Getafe ya ligi kuu nchini Hispania ambao waliomtaka nyota huyo kwa mkopo.

Nyota huyo hadi sasa ana goli 4 na pamoja na pasi 4 zilizo zaa magoli ligi kuu Misri amekuwa mchezaji muhimu sana kwenye kikosi cha Pyramids na sababu ya wao kugoma kumuachia ni malengo yao ya kuchukua ubingwa wa ligi kuu pamoja na klabu bingwa Afrika alisema kocha wao Krunoslav Jurcic.

Sababu kubwa ni malengo lakini kiuhalisia ni kwamba Klabu Inapesa za kutosha kumbakiza mchezaji wao maana ingekua timu nyingine wasingeweza kuweka ngumu kwa mchezaji wao.

Nini maoni yako kwa jambo walilolifanya Pyramids Timu anayocheza Mshambuliaji Fiston Mayele aliewahi kuwika na Timu ya Yanga Tanzania.