JKT Tanzania yashikwa shati na KenGold

JKT Tanzania kwenye uwanja wake wa nyumbani wa Meja Isamuyo uliopo Mbweni jijini Dar es Salaam imeshindwa kuondoka na ushindi baada ya kulazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 mchezo wa Ligi Kuu bara.

Walianza JKT Tanzania kupata bao la kuongoza kwa mkwaju wa penalti na mshambuliaji Edward Songo dakika ya 48.

KenGold walisawazisha kupitia kwa kiungo mshambuliaji wake Seleman Salim Rashid Bwenzi dakika ya 85.

Kwa matokeo hayo JKT Tanzania wamefikisha pointi 27 na michezo 22 wakishika nafasi ya 6 wakati KenGold wakiendelea kushika mkia lakini wakifikisha pointi 15 na michezo 22.