Simba yashindwa kuifunga Azam

Simba SC imeshindwa kuibuka na ushindi mbele ya Azam FC katika mchezo wa Ligi Kuu bara kwenye uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam usiku huu baada ya kufungana mabao 2-2.

Kwa matokeo hayo Simba imefikisha pointi 51 ikiwa na mechi 20 nafasi ya pili nyuma ya Yanga yenye pointi 55 mechi 21, wakati Azam FC imefikisha pointi 44 mechi 21 nafasi ya tatu.

Azam FC walitangulia kupata bao la kwanza kupitia Gibril Silla dakika ya 01 kabla Simba kusawazisha dakika ya 26 kupitia Elie Mpanzu, lakini Simba waliongeza bao la pili kupitia Abdulrazak Hamza dakika ya 75 kabla ya Zidane Sereli dakika ya 88 kuisawazishia Azam





Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FIFA yatoa orodha ya vilabu bora duniani, Simba na Yanga zachuana vikali

Beno Ngassa mdogo wa Mrisho Ngassa anayekipiga Tanzania Prisons

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI