Mzee Mchengelwa afariki dunia

Baba yake Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mohamed Mchengerwa, Alhaj Omary Mchengerwa amefariki leo Alfajiri akiwa kwenye Ibada ya Umrah huko Makka.

Kwa mujibu wa taarifa ya Familia ya Mchengerwa, Mzee Omary atazikwa leo huko huko Makka.

Ifuatayo ni Ratiba ya Ibada ya Visomo vitakavyoongozwa na Mufti wa Tanzania Dkt Zuberi Bin Ali wa Mbwana nyumbani kwa Waziri Mchengerwa, Masaki Dar es Salaam.

LEO: TAREHE 24 FEBRUARI 2025

Dua ya Kisomo itafanyika nyumbani kwa Mhe. Mohamed Mchengerwa Masaki saa 10 Alasiri

KESHO TAREHE: 25 FEBRUARI 2025

Dua ya kisomo itafanyika Jimboni Rufiji

KESHO KUTWA TAREHE: 26 FEBRUARI 2025

Dua itafanyika nyumbani kwake Marehemu Alhaj Omary Mchengerwa Yombo.


Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FIFA yatoa orodha ya vilabu bora duniani, Simba na Yanga zachuana vikali

Beno Ngassa mdogo wa Mrisho Ngassa anayekipiga Tanzania Prisons

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI