KenGold balaa, yamleta Luis Miquissone, Hussein Kazi naye ndani
Kama mazumguzo yatafikia mwisho mzuri tegemea kumuona Luis Miquisone ndani ya NBC Premier League kwenye hili dirisha dogo. Tajiri wa #Ken_Gold ameamua kushusha vyuma kuinusuru timu hiyo isirudi NBC Championship. Bado mazumguzo yanaendelea baina ya pande mbili. Luis Miquissone Wakati huo huo Ken Gold kutoka Chunya Mkoani Mbeya ipo kwenye mazungumzo na klabu ya Simba kwaajili ya kuipata saini ya beki wa kati Hussein Kazi ili kuongeza nguvu kikosini hapo. Hussein Kazi mkataba wake na Simba unamalizika Julai 2025, na hadi sasa hayupo kwenye mipango ya kocha Fadlu. Hussein Kazi